Wednesday, 26 February 2025

KAMISHNA WA KODI TRA AFANYA ZIARA YA DUKA KWA DUKA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA WILAYANI TUNDURU

 

RUVUMA

kamishna wa kodi za ndani kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) BW. Alfred Mregi amefanya ziara ya kuwatembelea wafanyabiashara wilayani tunduru mkoani Ruvuma katika maeneo yao ya biashara lengo likiwa ni kusikiliza maoni ,ushauri, na changamoto zinazowakumba wafanyabiashara wilayani humu  katika maeneo yao ya biashara




sambamba na hilo Bw. Mregi amefanya kikao na wafanyabiashara wa wilaya ya Tunduru ambapo timu ya wataalamu  kutoka  TRA walitoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara na baadae Kamishna aliweza kusiliza changamoto pamoja na maoni kutoka kwa wafanyabiashara.

Katika kikao hicho changamoto mbalimbali  zimetolewa na wafanyabiashara kuhusiana na kodi ambapo changamoto hizo zimetatuliwa kwa kutolewa ufafanuzi na kamshina wa kodi za ndani,

 



Pamoja na hayo Bw. Alfred Mregi amewaomba na kuwasisitiza wafanyabiashara  wilayani  Tunduru kufuata sheria zilizowekwa na serikali ili waweze kuondokana na changamoto za kikodi pamoja na kuepuka uonevu unaoweza kujitokeza kwa kutokujua sheria zinasemaje.

 

pia amewaomba wafanyabiashara kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania wilayani humo kwa  kushiriki  semina ili waweze kujifunza ni kwa namna gani sheria zinawataka wafanye aidha amesema TRA itaendelea kutoa semina na elimu ya kodi mara kwa mara ili kuwawezesha wafanyabiashara kusikilizwa na kupaia elimu ya kodi



No comments:

Post a Comment