Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Tulizo Mapunda, amekamilisha hatua ya awali ya mchakato wa kuwania nafasi ya
ubunge kwa kurejesha rasmi fomu ya kugombea katika ofisi ya CCM Wilaya ya
Mbinga.
Mapunda alichukua fomu hiyo tarehe
29 Juni 2025, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa ndani wa chama cha CCM wa kuwapata
wagombea watakaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
Mapunda anawania kupitishwa na chama chake ili kupeperusha
bendera ya CCM kwa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini.
Akizungumza mara baada ya kurejesha
fomu hiyo, Mapunda amewashukuru wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la
Mbinga Vijijini kwa ushirikiano waliompa tangu mwanzo wa safari yake ya kisiasa
Amesema kuwa ana nia thabiti ya kuleta maendeleo kwa
kushirikiana na wananchi, endapo atapewa nafasi ya kuwa Mbunge wa jimbo hilo.



No comments:
Post a Comment