Monday, 6 March 2017

Tanzanite: Diamond Platinumz alinibania Collabo kwa wasanii wengine

Hit maker wa nyimbo ya usinipite – Tanzanite amefunguka kwenye kipindi cha Home Boys Talk Show kinachoendeshwa na kurushwa na Rise Online Tv kuwa tofauti yake na Diamond Platinum ilisababisha akose ushirikiano toka kwa wasanii wengine

Tazama video hapo chini jinsi alivyo mwaga povu    


Licha ya hivyo ameweka wazi kuwa  uhusiano wake na Diamond haukuwa mzuri baada ya kuachia cover ya uchawi na wanga

“baada ya ile nyimbo mambo yaliendelea sio mazuri, japo kuwa  vingi vimeongelewa lakini mimi ndio muhusika naya yeye ndie muhusika, mambo hayakuwa mazuri changamoto zilikuwa ni nyingi, vikasemekana vitu vingi, wakaongea vitu vingi, nikaongea vitu vingi lakini mwisho wa siku nasimamia kuwa mambo hayakuwa mazuri ” alisema Tanzanite


Tanzanite kwa sasa ameachia kazi mpya aliyompa shavu king of vigoma Trap namzungumzia Dee Pesa kibao kinacho julikana kama Usinipite,
Usikose kutazama fully Interview ya Tanzanite katika kipindi chako bora cha Home Boys Talk Show na Mr 255 whitesam ndani  ya Rise Online Tv. 

Tazama Video Hapo Chini Tanzanite akiimba live nyimbo ya usinipite kwenye kipindi Home Boys Talk Show ndani ya Rise Online Tv.


No comments:

Post a Comment