Haijawa kitu rahisi kwa mbongo Fleva Ally Timbulo a.k.a Timbulo kushawishika na maneno ya Mpenzi wake wazamani (Ex Girl Friend) ambaye anatamani iwe kama zamani ambapo jamaa ameamua kumchana kwa kumtolea ngoma inayojulikana kwa jina la Mshuma
“Nimemuimbia EX wangu aliyeniacha ,
kunikimbia, aliyeniona si kitu na kunitafuta kutaka turudiane” alisema Timbulo wakati
akitambulisha wimbo wake mpya kwenye kipindi cha (Xtra Xtra Large) (XXL) Kubwa
kubwa kuliko kinachorushwa na The People Station Clouds Fm.
Pia Timbilo
amewasihi mashabiki wake kutokuwa na hofu dhidi ya mtindo wake mpya wa kutoa
nyimbo mfululizo na kusema haofii kukandamiza nyimbo nyingine.
“Sikandamizi miziki
wangu nawapa mashabiki wanachokitaka”
Ikumbukwe Miezi
micha iliyopita Timbulo aliachia ngoma ya Mfuasi pindi ikiwa inafanya vizuri katika soko la muziki na masikioni mwa watu
akaachia ngoma ya Ni wewe na pindi ikiwa
niaanza kueleweka kwa mashabiki ameudondosha ngoma ya Mshumaa.

No comments:
Post a Comment