| Kaimu
Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Boniface Mhabe kushoto akipokea msaada
wa mashuka 50 kutoka kwa Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Sub Agro
Trading anda Engineering,Neema Ng'unda kwa ajili ya wodi ya wakina mama
wajawazito kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza jana ilkiwa ni
kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika kilimo wa pili kutoka kushoto
ni Afisa Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao makuu yake mjini Arusha,Shillaga Samweli |
HOSPITALI
ya Teule wilayani Muheza Mkoani Tanga imepata msaada wa mashuka 50 kwa
ajili ya kukabiliana na uhaba uliopo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa
ya wagonjwa wanao kwenda kupata matibabu kutoka maeneo mbalimbali hasa
vijijini.
Hatua ya uhaba huo unatokana na uchakavu wa wa mashuka unaotokana na kufubaa
unaosababishwa na maji wanayotumia kufulia kutokana na uhaba wa maji
hali iliyopelekea kuwepo uhitaji kila wakati ili kuweza kukithi mahitaji
ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu.
Hayo yalibainishwa jana na Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza, Boniphace
Mhabe wakati akipokea msaada wa mashuka 50 kutoka kampuni ya Suba Agro
Trading na Engineering ambao ni mzalishaji wa mbegu bora zamahindi kwa
kushirikiana na Cimmity taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mahindi na
Ngano.
Shuka hilo zilitolewa kwa ajili ya wodi ya wakina mama wajawazito kwenye
hosptali ya Teule Muheza,Hospitali ya wilaya ya korogwe na ile ya
wilaya ya Handeni lengo kubwa likiwa kuwaondolea changamoto
zinazowakabili.
"Vitanda vipo vingi lakini tatizo kubwa ni mashuka na hili linatokana na
asilimia kub wa kuchakaa kutokana na maji lakini pia wakati mwengine
yanabadilika rangi jambo ambalo limekuwa changamoto kwao.
Aidha alisema wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kusaidia msaada huo ambao umefika wakati muafaka kwa kusadia baadhi ya vikwazo wanazokutana navyo wakati wa utoaji wa huduma za afya.
Awali akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Afisa Masoko na Mauzo
wa Kampuni hiyo,Neema Ng'unda alisema alisema wamekuwawakishiriki
katika kuhamasisha kilimo Tanzania hususani kwa wakina mama ambao ndio
nguzo kubwa hapa nchini kufikia mafanikio.
Alisema wamelenga wanawake kwa sababu ndio muhimili muhimu kwenye jamii wa kuwawezesha wakina baba kwenye kulima kilimo bora ambapo kinaweza kuwainua kiuchumi.
"Lakini pia tunawashukuru wakulima wote Tanzania kwa kutumia mbegu zao kwa kulima kilimo cha kisasa ambacho kinaweza kuwa mkombozi kijiinuakimaendeleo na kukuza mitaji yao "Alisema.
Naye kwa upande wake,Afisa Mauzo wa Suba Agro Trading yenye makao makuu
yake mjini Arusha,Shillaga Samweli alisema zoezi hili limelenga
kurudisha fadhila kwa wakina mama wa Tanzania maana ndio wamekuwa
wakishiriki kikamilifu katika kilimo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment