Shirika lisilo la kiserikali la Rise charity limezindua
kampeni iitwayo Mtoto kwanza Elimu ni Msingi Ambapo kampeni hiyo yenye dhumuni
la kuwasaidia watoto wa shule za msingi kwa kuwachangia vifaa mbalimbali
vitakavyo wawezesha katika Masomo .
Kampeni hiyo imezinduliwa kwa Mara ya kwanza katika mkoa wa Morogoro wilaya ya
kilosa kijiji cha Ngoisani ndani ya shule ya Mabwegere ikiwa ni kampeni
inayotarajiwa kuzunguka katika mikoa mbalimbali Tanzania.
Aidha wakati wa uzinduzi huo ulio ambatana na kutoa msaada wa vifaa vya
kujifunzia Katibu wa kampeni hiyo Atley Timothy Kayuni amewaasa watoto kwa
kusema
"Msaada huu umetolewa na watanzania na wapenda maendeleo hivyo muutumie
vizuri na kwamanufaa ya upataji elimu bora ambayo itawasaidia mbeleni katika
maisha hivyo mkazane ili kutimiza ndoto zenu" alisema Kayuni
Naye Mmoja wa walimu katika shule hiyo Mwl. Mbapila amelishukuru shirika hilo
kwa kuwakumbuka na kwenda kuwaona na kusema ni watu wachache sana wenyemoyo wa
kujitolea hivyo wasichoke kutoa kwani shule ni nyingi na nyingi zinahari mbaya
hususani vijijini.
| Katibu wa kampeni ya "Mtoto kwanza elimu ni msingi" Atley T Kayuni akitoa somo kwa wanafunzi wa shule ya msingi mabwegere kabla yakutoa msaada kwa wanafunzi hao. |
| Mkurugenzi Mtendaji wa Rise Media Innocent Horomo akitoa msaada wa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi, ikiwa ni kampeni inayoendeshwa na Rise Charity. |
Afisa habari wa Rise Media ambae pia ni mwakilishi wa Rise
Charity akiteta jambo na wanafunzi wa shule ya msingi mabwegere wakati wa zoezi
la uzinduzi wa kampeni ya Mtoto kwanza elimu ni msingi
|
| Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi mabwegele wakiwa darasani wakati wa zoezi la kampeni ya Mtoto kwanza elimu ni msingi |
| Mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mabwegere akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Rise Charity kwa kuwakumbuka na kuwapa msaada |
| Wanafunzi wakifurahia msaada waliopewa kwa kunyosha juu vifaa vya kujifunzia |
(Picha Zote na Rise Production)
No comments:
Post a Comment