Tuesday, 1 July 2025

KADA WA CCM TULIZO MAPUNDA AREJESHA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MBINGA VIJIJINI

 

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tulizo Mapunda, amekamilisha hatua ya awali ya mchakato wa kuwania nafasi ya ubunge kwa kurejesha rasmi fomu ya kugombea katika ofisi ya CCM Wilaya ya Mbinga.

Mapunda alichukua fomu hiyo tarehe 29 Juni 2025, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa ndani wa chama cha CCM wa kuwapata wagombea watakaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.

Mapunda anawania  kupitishwa na chama chake ili kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini.

Leo, tarehe 01 Julai 2025, Mapunda amerudisha rasmi fomu hiyo, hatua inayodhihirisha dhamira yake ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Mbinga Vijijini endapo atapewa ridhaa na chama na hatimaye kushinda uchaguzi.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu hiyo, Mapunda amewashukuru wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Mbinga Vijijini kwa ushirikiano waliompa tangu mwanzo wa safari yake ya kisiasa

Amesema  kuwa ana nia thabiti ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi, endapo atapewa nafasi ya kuwa Mbunge wa jimbo hilo.

Tuesday, 22 April 2025

TİKA, SONGEA İLÇESİNDE 55 KALKINMA GRUBUNA MISIR DEĞER KATMA MAKİNELERİ SAĞLIYOR

 


Tanzanya'nın Ruvuma bölgesindeki Songea İlçesi’ne bağlı 18 köyden gelen yaklaşık 55 kalkınma grubu, Türk İşbirliği ve Koordinasyon Ajansı Başkanlığı (TİKA) tarafından sağlanacak mısır ürünlerine değer katma makinelerinden faydalanacak.

Bu destek kapsamında, 23 gruba mısır öğütme ve kabuk soyma makineleri, 32 gruba ise mısır ayıklama makineleri verilecek.

TİKA Tanzanya Program Koordinatörü Filiz Şahinci, bu grupları ziyaretinde yaptığı konuşmada, ajansın hedeflerinden birinin, özellikle kadınları hedef alarak, ekonomik zorluklarla mücadele eden düşük gelirli bireyleri desteklemek olduğunu ifade etti. Şahinci, “Bir kadın ekonomik olarak güçlenirse, tüm toplum güçlü olur,” dedi.


Peramiho Milletvekili ve aynı zamanda Tanzanya Sağlık Bakanı olan Sayın Jenista Mhagama ise, TİKA’nın Cumhurbaşkanı Dr. Samia Suluhu Hassan liderliğindeki Altıncı Hükümet ile işbirliği içinde Tanzanya halkının kalkınmasına yönelik katkılarını takdir ettiğini belirtti. Mhagama, bu makinelerden faydalanacak vatandaşlara, tarımsal üretime devam etmeleri ve elde ettikleri bu fırsatları en iyi şekilde değerlendirmeleri çağrısında bulundu.

İktidar partisi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Başkanı Thomasi Maswolwa ise, vatandaşlara kalkınma ortakları bulma çabalarının CCM’nin Seçim Beyannamesi’nin uygulanmasının bir parçası olduğunu belirtti. Aynı zamanda ülkede mevcut olan barış ve istikrarın, TİKA gibi uluslararası iş birliklerini mümkün kıldığını vurguladı.




Yardımı alan vatandaşlar, TİKA’ya ve milletvekili ofisine kalkınma gruplarının önemini tanıdıkları için teşekkür etti. Bu desteğin, özellikle mısır ürünlerinin değerini artırarak, grupların ve bireylerin ekonomik olarak güçlenmelerine büyük katkı sağlayacağı ifade edildi.


TIKA KUTOA MASHINE ZA KUONGEZA THAMANI KWA MAHINDI KWA VIKUNDI 55 JIMBO LA PERAMIHO


Takriban vikundi 55 vya maendeleo kutoka kata 18 ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma, vinatarajiwa kunufaika na mashine za kuongeza thamani ya zao la mahindi zitakazotolewa na Shirika la Kiserikali la Uturuki (TIKA).

Katika ufadhili huo, vikundi 23 vitapokea mashine za kusaga na kukoboa mahindi, huku vikundi 32 vikipewa mashine za kupukuchua mahindi.

Filiz Sahinci, Mratibu wa Programu za TIKA nchini Tanzania, akizungumza katika ziara ya kutembelea vikundi hivyo, amesema moja ya malengo ya shirika hilo ni kuwawezesha wananchi wa hali ya chini kiuchumi kwa kuwasaidia katika changamoto mbalimbali zinazowakwamisha kiuchumi hasa wakiwa wamelilenga kundi la wanawake, amesema kuwa “Mwanamke akiwa na nguvu ya kiuchumi, jamii nzima itakuwa na uchumi imara.”




Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, amelipongeza shirika la TIKA kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

Mhe. Mhagama ametoatoa wito kwa wananchi wanaonufaika na mashine hizo kuendelea kujikita katika uzalishaji wa mazao na kuzitumia vyema fursa walizopata ili kujikwamua kiuchumi.

Naye Thomasi Maswolwa, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema jitihada za kuwatafutia wananchi wadau wa maendeleo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Ambapo pia amesisitiza umuhimu wa kutunza amani na utulivu uliopo nchini ambao umewezesha ushirikiano wa kimataifa kama huu kutoka TIKA.





Wananchi waliopokea msaada huo wamelishukuru shirika la TIKA na Ofisi ya Mbunge kwa kutambua umuhimu wa vikundi vya maendeleo. Walisema msaada huo utasaidia sana vikundi na wanachama mmoja mmoja katika kujikwamua kiuchumi na kuongeza thamani ya mazao yao, hasa mahindi.

Wednesday, 26 February 2025

KAMISHNA WA KODI TRA AFANYA ZIARA YA DUKA KWA DUKA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA WILAYANI TUNDURU

 

RUVUMA

kamishna wa kodi za ndani kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) BW. Alfred Mregi amefanya ziara ya kuwatembelea wafanyabiashara wilayani tunduru mkoani Ruvuma katika maeneo yao ya biashara lengo likiwa ni kusikiliza maoni ,ushauri, na changamoto zinazowakumba wafanyabiashara wilayani humu  katika maeneo yao ya biashara




sambamba na hilo Bw. Mregi amefanya kikao na wafanyabiashara wa wilaya ya Tunduru ambapo timu ya wataalamu  kutoka  TRA walitoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara na baadae Kamishna aliweza kusiliza changamoto pamoja na maoni kutoka kwa wafanyabiashara.

Katika kikao hicho changamoto mbalimbali  zimetolewa na wafanyabiashara kuhusiana na kodi ambapo changamoto hizo zimetatuliwa kwa kutolewa ufafanuzi na kamshina wa kodi za ndani,

 



Pamoja na hayo Bw. Alfred Mregi amewaomba na kuwasisitiza wafanyabiashara  wilayani  Tunduru kufuata sheria zilizowekwa na serikali ili waweze kuondokana na changamoto za kikodi pamoja na kuepuka uonevu unaoweza kujitokeza kwa kutokujua sheria zinasemaje.

 

pia amewaomba wafanyabiashara kuendelea kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania wilayani humo kwa  kushiriki  semina ili waweze kujifunza ni kwa namna gani sheria zinawataka wafanye aidha amesema TRA itaendelea kutoa semina na elimu ya kodi mara kwa mara ili kuwawezesha wafanyabiashara kusikilizwa na kupaia elimu ya kodi



Tuesday, 4 February 2025

WANACHAMA WA CCM WILAYA YA SONGEA, VIJIJINI JIMBO LA MADABA WAMUNGAMO MKONO AZIMOAMKUTANO MKUU MAALUMU CCM TAIFA

 


Katika sherehe za miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanachama wa CCM kutoka Wilaya ya Songea Vijijini, Jimbo la Madaba, wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Thomas Masolwa, wamepongeza na kuunga mkono Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa, uliopitisha azimio la kumteua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa Tanzania Bara, huku Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiteuliwa kugombea urais kwa upande wa Zanzibar.



Akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Jimbo la Madaba waliojitokeza kusherehekea miaka 48 ya CCM katika kijiji cha Lutukila kilichopo kata ya Mkongotema, Masolwa alieleza furaha ya wanachama wa CCM Jimbo la Madaba kutokana na mafanikio makubwa yaliyofikiwa chini ya uongozi wa Rais Samia. Ametaja maendeleo katika sekta za afya, elimu, miundombinu, kilimo na huduma nyingine za kijamii ambazo zimeboresha maisha ya wananchi, hasa wa vijijini.

Aidha wanacha hao wamempongeza na kuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho taifa kwa kumchagua Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa CCM, kama mgombea mwenza katika uchaguzi ujao.

Masolwa amewataka Wananchi wa Jimbo la Madaba kuendelea kuiunga mkono CCM kwa kumchagua Rais Samia na viongozi ngazi ya ubunge na udiwani watakaoteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera ya chama  katika uchaguzi ujao



Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini, Juma Nambaila, amesema kuwa maadhimisho ya miaka 48 ya CCM yameambatana na shughuli mbalimbali za kijamii, zilizofanywa na jumuiya za chama ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira, na uchangiaji damu,

Mbunge wa Jimbo la Madaba, Dkt. Joseph Mhagama, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia kwa kutekeleza miradi ya maendeleo katika jimbo hilo. Amesema wananchi wa Madaba wanapata manufaa makubwa kutokana na serikali yao kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali ya chama cha mapinduzi ikiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Sherehe hizi zimeonyesha mshikamano wa wanachama wa CCM, huku wakiahidi kuendelea kuiunga mkono CCM na Rais Samia katika kipindi cha uongozi wa Awamu ya Sita.

 


Sunday, 26 January 2025

DC UVINZA AMEWATAKA MAAFISA UTUMISHI KUWAJIBIKA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO

 


Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Bi.Dina Mathamani amewataka maafisa Utumishi wa Wilaya hiyo kuwajibika katika kutekeleza majukumu yao pindi wanapowatumikia  Wananchi kwa kuibua changamoto wanazokutana nazo katika maeneo yao.

Hayo yamejiri katika mafunzo ya Elimu ya uraia na utawala bora yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza mkoani Kigoma.

Akizungumza katika mafunzo hayo Bi.Mathamani amesema kuwa ili watumishi hao waweze kufanya shughuli zao vizuri ni lazima suala la utawala bora liweze kuzingatiwa ili wananchi wajue vitu wannavyovihitaji katika nchi yao.




Kwa upande wake Bw.Hamis Mjanja kutoka ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI amesema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kukumbusha wajibu wa kila kiongozi katika utekelezaji wa majukumu aliyopewa na serikali .

Bw.Mjanja Amesema kuwa ni muhimu kwa viongozi wa serikali kufanya kazi kwa kuzingatia suala la utawala bora

Nao baadhi ya washiriki waliohudhuria akiwemo Hedetrides na Frank Michael ambao ni watendaji wa kata wamesema mafunzo hayo wamesema mafunzo waliyopata leo watayafanyia kazi kwa kuzingatia misingi na weledi hususani katika suala la utawala bora na sheria.



Mafunzo hayo yanayoratibiwa na wizara ya katiba na sheria yameshafanyika katika mikoa mitano na kwasasa yanaendelea kufanyika katika mikoa sita na hivyo kukamilika kwake kutaongeza idadi na kufanya mikoa kumi na moja kuwa imefikiwa na mafunzo haya.

Mikoa ambayo mafunzo hayo yanafanyika kwa sasa ni pamoja na mkoa mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro, Geita, Katavi, Tabora na Mtwara

Thursday, 19 December 2024

TRA Yatoa Wito Kwa Wafanyabiashara Kujitokeza Kushiriki Katika Maboresho Ya Sheria Ya Kodi

 

Mkurugenzi wa Elimu na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo, amewaasa wafanyabiashara nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la ukusanyaji na utoaji wa maoni ya maboresho ya kodi kwa ajili ya maandalizi ya sharia ya  kodi kwa mwaka mpya wa fedha wa 2025/26.
Mkurugenzi wa Elimu na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akizungumza na wafanyabiashara wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma


Kayombo alitoa wito huu akiwa wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma, katika semina iliyohusisha wafanyabiashara, ambapo pia ilifanyika utoaji wa elimu kuhusu mlipa kodi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara. Katika semina hiyo, Kayombo alisisitiza kuwa serikali kwa sasa ipo katika zoezi la ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wafanyabiashara ili kuboresha mfumo wa kodi na mazingira ya biashara nchini.

"Serikali inajitahidi kuboresha mazingira ya biashara, na zoezi hili la ukusanyaji maoni ni muhimu ili kubaini changamoto zinazowakabili wafanyabiashara biashara," alisema Kayombo. Aliongeza kuwa, wafanyabiashara wanapaswa kutoa maoni yao kupitia vyombo vya wafanyabiashara na chemba mbalimbali katika maeneo yao ili kusaidia kufikia malengo ya kuboresha mfumo wa kodi na kupunguza malalamiko kutoka kwa jamii ya wafanyabiashara.


Aidha, Kayombo alisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kulipa kodi kwa hiyari, akieleza kuwa njia hii itasaidia kuongeza mapato ya serikali, hivyo kuweza kuendelea kuwahudumia wananchi kwa huduma bora. "Ikiwa wafanyabiashara wataendelea kulipa kodi kwa hiyari, serikali itaweza kuwekeza katika maendeleo ya jamii na kutoa huduma muhimu," alisisitiza Kayombo.

Semina hii ni sehemu ya juhudi zinazofanywa na TRA na serikali kwa ujumla kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanapata elimu ya kutosha kuhusu masuala ya kodi na kusaidia kuboresha mazingira ya biashara nchini.