Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani
Kigoma Bi.Dina Mathamani amewataka maafisa Utumishi wa Wilaya hiyo kuwajibika
katika kutekeleza majukumu yao pindi wanapowatumikia Wananchi kwa kuibua changamoto wanazokutana
nazo katika maeneo yao.
Hayo yamejiri katika mafunzo ya
Elimu ya uraia na utawala bora yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya
ya uvinza mkoani Kigoma.
Akizungumza katika mafunzo hayo
Bi.Mathamani amesema kuwa ili watumishi hao waweze kufanya shughuli zao vizuri
ni lazima suala la utawala bora liweze kuzingatiwa ili wananchi wajue vitu wannavyovihitaji
katika nchi yao.
Kwa upande wake Bw.Hamis Mjanja
kutoka ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI amesema kuwa
lengo la kufanya mafunzo hayo ni kukumbusha wajibu wa kila kiongozi katika
utekelezaji wa majukumu aliyopewa na serikali .
Bw.Mjanja Amesema kuwa ni muhimu
kwa viongozi wa serikali kufanya kazi kwa kuzingatia suala la utawala bora
Nao baadhi ya washiriki
waliohudhuria akiwemo Hedetrides na Frank Michael ambao ni watendaji wa kata
wamesema mafunzo hayo wamesema mafunzo waliyopata leo watayafanyia kazi kwa
kuzingatia misingi na weledi hususani katika suala la utawala bora na sheria.
Mafunzo hayo yanayoratibiwa na
wizara ya katiba na sheria yameshafanyika katika mikoa mitano na kwasasa
yanaendelea kufanyika katika mikoa sita na hivyo kukamilika kwake kutaongeza
idadi na kufanya mikoa kumi na moja kuwa imefikiwa na mafunzo haya.
Mikoa ambayo mafunzo hayo
yanafanyika kwa sasa ni pamoja na mkoa mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro, Geita,
Katavi, Tabora na Mtwara




No comments:
Post a Comment