Tuesday, 11 July 2017

2 Chainz amtaja JAY-Z kuwa ni mwanamuziki anayetamani kurekodi naye ngoma

Mwanamuziki  ambaye pia ni Rapa anaye julikana kwa jina la 2 Chainz kwa sasa anaitangaza  album yake mpya  inayokwenda kwa jina la Pretty Girls Like Trap Music,  amefunguka na kumtaja msanii anayetaka kufanya naye kazi kabla hajastaafu  shughuli zake za muziki.

2 Chainz ambaye tayari ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kama  vile Kanye West na wengine kibao, amemtaja  Rapa JAY-Z kuwa ni msanii anayetamani kufanya naye kazi katika ngoma yak yoyote ile  kabla hajastaafu muziki.


Chainz amesema, Rapa JAY-Z ni mtu wa kwenda na wakati kwani wanaendana sababu wote wanabadilika kulingana  na wakati.

No comments:

Post a Comment