Chama cha wabunifu na watengenezaji wa vifaa mbalimbali vya walemavu(DAGE),kimemwomba
Waziri waSera,Bunge,Kazi Ajira, Vijana na Walemavu Jenista Mhagama,kuwa nunulia
mashine za kutengenezea maumbo mbali mbali ya vifaa vya walemavu.
Ombi hilo lilitolewa jana na Katibu Mtendaji wa chama hicho
Patrick Mdachi, ambapo alisema mashine walionayo kwa sasa ni ya zamani na haina
uwezo wakutengeneza baiskeli 35 kwa mwezi.
“Kwa kipindi kirefu tumekuwa tuki pata shida wakati watu wanapo kuja
kuleta tenda ya kuwa tengenezea baiskeli za aina tofauti tofauti za walemavu
ambapo tunashindwa kutengeneza kwa haraka na mashine hiyo
imechoka alisema.”Mdachi
Alisema mashine hiyo inazaidi ya miaka 10 tangu ianze kufanya kazi na
wakati mwingine wanalazimika kuitengeneza ili iweze kufanya kazi.
Mdachi alisema kutokana tatizo hilo wamekuwa
wakishindwa kutengeneza baiskeli nyingi ambazo zinauhitaji mkubwa kwa baadhi ya
walemavu.
“kwa kipindi cha cha nyuma kwa mwezi mmoja
tulikuwa tunatengezena baiskeli 35 kiasi lakini sasa tunashindwa
kufikia kiwango hicho kutokana na mashine hiyo kusumbua alisema,”Mdachi
Pia alisema kumekuwepo na wimbi la baadhi ya mafundi mitaani
wanaowatengenezea walemavu baiskeli ambalo zinashindwa kukidhi mahitaji yao
pamoja na kuhalibika kwa kipindi kifupi.
“Kitendo cha baadhi ya watu wasio kuwa kuwa walwmavu
kutengeneza vifaa hivyo wanakuwa hawanaujuzi wakujua wanatakiwa
wawekewe vitu gani ukiachana na sisi walemavu,” alisema Mdachi
Alisema mara kwa mara wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya
walemavu juu ya ubora wa baiskeli hizo wakiulizwa
wanasema wanasema walizipata katika chama hicho jambo ambalo halina ukweli.
Afisa miradi wa chama hicho Henry Chacha alisema kuna
watu wanachukua kazi za kutengeneza vifaa hivyo bila kuwa na taaluma nayo
jambao ambalo linawasumbua walemavu wengi,
“Walemavu iliwaachane na kukaa mitaani na kuomba lazima wapate vifaa vya
kuwa saidi ambapo unakuta wananunua vifaa hivyo kwa bei kubwa.”alisema
Chacha
Pia aliiomba
serikali kuwaongezea wataalamu katika
chama hicho ilikupata ubunifu zaidi wa kutengeneza
vifaa mbalimbali za walemavu.
No comments:
Post a Comment