
Msanii
wa muziki, ambaye ni Mbunge wa Mikuni kupitia tiketi ya chama cha
CHADEMA, Joseph Haule maarufu kama Professa Jay, yupo matatani kukosa
hifadhi ya jumba lake la kifahari alilojenga pembezoni mwa barabara ya
Morogoro maeneo ya Mbezi Luis, kwani ni miongoni mwa nyumba ambazo
zimewekewa alama ya X kuashiria zipo katika hifadhi ya barabara.
Na nyumba ya Mbunge wa Mikumi ni moja ya nyumba ambazo zimewekewa X kuashiria nayo imo miongoni mwa nyumba za kubomolewa.
Hivi karibuni Tanroads imetangaza kuwa muda wowote itaanza utekelezaji
wa kubomoa nyumba zilizowekewa alama ya X katika barabara hiyo kupisha
ujenzi wa barabara kubwa ya kisasa.
Tayari Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limeshaanza kukata umeme kwenye
nyumba nyingi hivyo kuwafanya baadhi ya wenye nyumba kubomoa wenyewe
kwa hiari na kufungasha mizigo yao.
Tazama picha ya nyumba ya kifahari ya mbunge wa Chadema Joseph Haule
maarufu kama Profesa jay ambaye hivi karibuni alifunga harusi kubwa na
kuweka jiko ndani.


No comments:
Post a Comment