Mkurugenzi
Msaidizi wa Ufatiliaji na Tathimini wa CAG, Wendy Masoyi akizungumza
katika ufunguzi wa warsha warsha ya Nne ya Asasi zisizo za Kiserikali na
waandishi wa habari katika kupata toleo maalum kwa mwaka wa fedha
ulioshia Juni 30, 2016 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa kitengo cha mawasiliano serikalini wa Ofisi ya CAG, Sarah Reuben
akineonesha muundo wa kitabu cha machapisho ya ukaguzi wa CAG kwa mwaka
ulioshia Juni 30 ,2016 kwa wana warsha hawapo pichani iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi
wa Serikali za Mitaa wa CAG Temeke, Angel Moshi akitoa mada kwa wana
warsha hawapo pichani juu ya miradi mbalimbali iliyoangaliwa katika
ukaguzi wa CAG kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 30 , ilifanyika jijini
Dar es Salaam.
Sehemu
ya wadau wakifatilia taarifa katika warsha ya toleo maalum kwa mwaka wa
fedha ulioshia Juni 30 ,2016 iliyohusisha Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani
pamoja na Dar es Salaam.
Picha
pamoja wadau katika warsha ya toleo maalum kwa mwaka wa fedha ulioshia
Juni 30 ,2016 iliyohusisha Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani pamoja na Dar
es Salaam.
OFISI
ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) imebainisha kuwa
kipengele cha kutotambua marekebisho ya sheria kilichomo kwenye mikataba
ya madini kimekuwa kikichangia kutoonekana kwa mabadiliko katika sekta
hiyo.
Hayo
yamebainishwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Nje wa ofisi ya CAG,
Johannes Kisiri wakati wa kutoa mada kuhusu ukaguzi wa hesabu za
mashirika ya umma katika sekta ya gesi kwenye warsha ya asasi za kiraia
na waandishi wa habari, amesema mikataba mingi ya madini na gesi kuna
kipengele ambacho sio muafaka kwa faida ya taifa ambacho kinasema ‘
yatakayobadilika kwenye sheria hayataathiri makubaliano ya awali,”
amesema
Kisiri
amesema ukaguzi umegundua kuwa Kampuni ya Tanzanite One Tanzania
Limited(TML) iliyoingia mkataba wa kuchimba madini ya tanzanite na
Shirika la Madini la Taifa(Stamico) imekuwa ikiizuia madini hayo kampuni
ya Sky Associates Vila ya bila kuishirikisha stamico.
Amesema
ushauri wa CAG kuhusiana na mradi kuazalisha umeme katika Korongo la
Stiegler ambao ulikuwa unasimamiwa na Mamlaka ya Uendelezaji Bonde la
Rufiji (RUBADA) umefanyiwa kazi kutokana ripoti ya CAG ilianisha kuwa
RUBADA haikuwa na uwezo wa kifedha wa kuenesha mradi huo na kushauri
kufanywa na taasisi za umma zenye uwezo kama tanesco,” amesema
Mradi
huo ambao ungekuwa na manufaa sana kwa gharama za dola za marekani
bilioni 2.4 (sawa na Sh trilioni 6) na kutakiwa kuzalisha megawati 2,100
ambapo Bunge limefuta sheria iliyoanzisha RUBADA kupisha taasisi
nyingine kuendesha mradi huo.
Mradi
huu ulipangwa kutekelezwa katika vipindi vya awamu tatu, ambapo awamu
ya kwaza ungezalisha megawati 300, ya pili 600 na awamu ya mwisho ni
megawati 300 ambayo ingekamilika mwaka 2028.
Kisiri
amesema mikataba inailazimisha tanesco kununua umme kwa Sh 544.65 kwa
uniti moja kutoka kampuni binafsi na kuuza kwa Sh 279.35 kwa uniti
No comments:
Post a Comment