Ufikivu
habari ni haki ya msingi. Inawawezesha wanawake na wanaume kuelewa na
kushiriki katika kujenga na kushirikiana ujuzi wanaohitaji ili watoe
mchango kikamilifu katika jamii yao. Raia wenye taarifa sahihi huifanya
serikali iwajibike.
Ufikivu
Habari ni dereva wa uvumbuzi na ubunifu, kuongeza fursa kwa wote, hasa
kwa wasichana na wanawake. Ufikivu habari huanza na kujitolea kwa
Serikali kutengeneza, kueneza na kutekeleza sera na sheria zinazohusu
haki ya habari na kuhakikisha kuheshimiwa kwa haki hii ya kibinadamu.
Hii inahitaji utaratibu wa ufanisi wa utekelezaji na utamaduni wa uwazi
katika aina zote za taasisi.
Wananchi
wanahitaji pia kuwa na fikra pana, ujuzi wa kusoma na ujuzi wa
kidigitali ambao unahitajika kufikia, kuchambua na kutumia habari kwa
njia tofauti, nje na ndani ya mitandao. Hii ndiyo maana UNESCO inaziomba
serikali zote na washirika kutumia uwezo wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano ili kusaidia kufikia Lengo la 4, Elimu Endelevu inayolenga
kuhakikisha "elimu shirikishi, sawa na ya ubora na kukuza fursa
za elimu isiyo na mwisho kwa wote; Ufikivu wa Habari pia unajumuisha
kukuza uandaaji wa maudhui yanayofaa, yenye kulenga jamii husika na
yanayopatikana kwa lugha mbalimbali. Yote hii inahitaji sera zenye
ufanisi na ushirikiano mzuri katika ngazi zote.
Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote pia ni fursa ya kurejea
ahadi yetu ya uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari.
Vyombo vya habari huchukua nafasi muhimu katika kuwezesha ufikivu wa
habari kwa wananchi na katika kufuatilia masuala muhimu ya kijamii na
wakati huo huo vikiwaelimisha wafuatiliaji kwa kuwapa ufahamu na ujuzi.
Haiwezekani
kuwepo kwa ufikivu wa habari kwa wote bila kuwepo kwa vyombo vya habari
vilivyo huru. Ufikivu wa habari sio tu ni lengo peke yake; pia ni
mchangiaji muhimu katika utekelezaji wa malengo mengine yote ya
Maendeleo Endelevu. Kwa hiyo ni muhimu tuendeleze juhudi zetu ili
kuhakikisha kuwa kila mwanamke na mwanamume wanafurahia ufikivu kamili
wa habari.
No comments:
Post a Comment