Na Mwandishi Wetu
Akizungumza Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo (TASUBA), Dakt. Harbert Makoye alisema
Tamasha hilo kongwe la burudani linatarajiwa kuanza Septemba 23 na kumalizika 30.
"Kauli mbiu ya tamasha kwa mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni katika kupiga vita Madawa ya kulevya" alisema.
Aliongeza Tamasha hili lengo ni kukutanisha wasanii mbalimbali wa ndani c nje ya nchi kuonyesha sanaa na kubadilishana uzoefu kwa dhumuni la kuboresha sanaa nchini.
Alisema katika kutambua umuhimu wa kubadilishana uzoefu tamasha waandaaji wa tamasha hilo wamealika vikundi kutoka mataifa mbalimbali ili kunogesha tamasha hilo kwa mwaka huu.
"Tunategemea kua na vikundi 68 na vinaendelea kuongezeka huku kukiwa na maonesho kutoka Zimbabwe ambapo tutapata kuona uasili wa Zimbabwe pia Ufaransa na Uingereza" alisema.
Makoye Alisema katika siku za tamasha hilo kutakua na maonesho ya mchana na jioni tofauti na miaka ya nyuma ambapo yalikua yanafanyika mchana tu.
"Safari hii tumepeleka mialiko kwenye shule za msingi na sekondari ili waweze kupata fursa kujifunza sanaa na utamaduni na hata shule ambazo hatuja waalika wafike" alisema.
Mwenyekiti wa Tamasha hilo John Mponda alisema mbali na burudani hiyo kutakua na mafundisho ya elimu ya kilujikinga na madawa ya kulevya, jamii kujitambua na Uzalendo.
Aliongeza Kutakuwa na sanaa ya ujasiliamali ambapo vijana watapata fursa kuuza bidhaa zao za sanaa, dawa lishe, picha na nk.
"Walengwa sana ni vijana na wanafunzi watatoa kiingilio cha sh 500 wakati watu wazima ndani ya Afrika mashariki 3000 na nje ya Afrika mashariki 5000" alisema.

No comments:
Post a Comment