Wednesday, 12 July 2017

Beach Soka Yatimba Uswazi


Na. William Kange

Dar es salaam 

Mchakato wa zoezi la kuwasaka wachezaji wenye vipaji wakuli sakata kabumbu katika mchezo wa soka la ufukweni “Beach soccer” bado linazidi kushika hamasa kubwa huo ambapo zoezi hilo lahami kwa wachezaji wenye vipaji waliopo mtaani kwa ngazi ya vilabu  baada ya muda mrefu kuhusisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali kutoka Dar es salaam.


Akizungumza  hii leo kwa njia simu na rise media kocha mkuu wa timu ya taifa  John Mwansasu ameeleza kuwa bado tarehe rasmi ya kuanza mchakato wa zoezi hii haijawekwa wazi kutoka na kukosa wadhami wakuweza kuendesha program ya kuwasaka wachezaji hao.
Amesema,  kwa sasa wameamua kujidhatiti kutoka wanafunzi vyuo muda mwingi wanakuwa kwenye masomo hivyo wanawakosa hususani wanapo kabiliwa na maandalisi ya kujiandaa na mashindano mbalimbali ya kimataifa.

“punde yatakapokuwa tayari tutawangazia kwasababu bado tunaongea na udhamini kwaajili ya kuendesha program hii kwa ngazi ya vilabu kwa mkoa wa Dar es salaam”alisema mwansasu

Ameongeza kuwa program hiyo yenye lengo la kuwasaka wachezaji watakao unda kikosi cha timu taifa kwa mchezo huo ambapo pia wanatarajia kuwafikia  wachezaji kutoka mikoa mbalimbali nchini watakao kujakuwa msaada wa timu ya taifa kwa siku za usoni

“mchezo huu unaitaji asili mali fedha hivyo yanahitajika maandalizi ya kutosha ilikuusambaza mchezo huu kwa hapa nchini”alisema mwansasu


Tazama hapo chini  kocha mkuu wa timu ya taifa  John Mwansasu akielezea kuhusu mchakato wa kusaka vipaji vya mchezo wa mpira wa miguu wa ufukweni

No comments:

Post a Comment