Wednesday, 12 July 2017

Ukata wa Kifedha Waikumba Riadha Nchini


Na. William Kange

Dar EsSalaam

Serikali imeobwa kuwasaidi  wanaridha juu ya hali inayo wakabili ya ukata wa kifeha iliwaweze kufanya vizuri  wanapoenda  kuwakilisha nchi  kwenye mashindano mbalimbali ya kidunia yanayo husisha riadha.

Ombi hilo limetolewa hii leo katibu mkuu wa shirikisho la riadha RT Wilhem Gudabuday wakati akizungumza na Rise Media  ambapo amemuomba waziri mwenye dhama ya michezo Mhe. Harrison George Mwakyembe kuwa awatazame wanariadha hao kwakuwa wao kama shirikisho wanakabiliwa na changamoto ya kifedha .
katibu mkuu wa shirikisho la riadha RT Wilhem Gudabuday
“tunakabiliwa na ukawa kiuchumi Hakuna pesa kwenye riadha tume tuma ‘proposal’ kwenye wizara  yenye dhamana bado tunasubili majibu”alisema Gidabuday   
Gidabudy amefunguka akisema mashindano yaliopo mbele yao  ambayo  makubwa matatu   ngazi ya kidunia ni mashindano ya junior ya Nairobi, ambapo wanariadha 12 wanatarajia kushiriki waliofikia viwango.

Amesema, pia kuna mashindano ya jumuhiya ya madola  ya “under eighteen (18 )” yatakayofanyika nchini Bahama yatashirikisha wanariadha 2 kutokaTanzania.
Wanariadha wa Tanzania wakishangilia mara baada y kushinda mbio za kupokezana vijiti
Ameongaza, vilevile kuna wanariadha ambao mpaka sasa wapo kambini Arusha kwa ajili kujiandaa na mashindano “ senior” yatakayo fanyika jijini London “Uingereza”.

 Aidha Gidabuday amewataja miongoni mwa wanariadha watakao wakirisha nchi kwenye mashindano  hayo ya London  akiwemo Alphonce Simbu,Saidi Makula,Magdalena Salumu,Ezekiel Mwangimba pamoja na Sarah Ramadhanl

No comments:

Post a Comment