Dar es Salaam
Uongozi wa klabu ya wakata miwa kutoka
morogoro“ Mtibwa sugar” umesema hawautambui usajili wa beki wa kati wa klabu
hiyo Salim Mbonde kwenda Simba kwa kuwa klabu hiyo imekiuka kanuni na utaratibu
wa usajili kwani klabu Mtibwa bado inamkataba na mchezaji huyo.
Akizungumza na Rise Media msemaji mkuu
wa klabu hiyo Thobias Kifaru ameutupia lawama uongozi wa klabu simba kwa
kukiuka sheria na kanuni za kwakile kilicho onekana kwenye mitandao ya kijamii
ikimuonesha beki wa kati wa klabu hiyo Salim Mbonde akimwaga wino kunako kablu
hiyo.
“Bado haijawa rasmi na sisi tumesikia
tu tuna tegemea simba kujakufanya
mazungumzo ndipo hapo mbonde atakapo tambulika mchezaji halali wa samba”
alisema kifaru
Katika hatua nyingine Kifaru amuzungumzia maandalizi ya Mtibwa Sugar
kuelekea ligi kuu Tanzania bara ambapo klabu hiyo imeanza kambi yake hii leo
Jiji Dar es salaam ambayo itadumu kwa wiki mbili itayomalizika July 29, na
inatarajia kucheza mchezo wa mechi ya kirafiki dhidi ya Mbeya City itayopigwa
kwenye uwanja wa Jamuhuri Mkoani morogoro
“
kambi yetu itaanza julai 12 ampaka 29 ilikujiandaa na ligi kuu ilikujiimalisha
tukiwa tuna malengo ya kuwa mabingwa kwa msimu wa mwaka 2017/2018”alisema
kifaru
Kipute cha ligi kuu Tanzania bara
kinatajia kutimua vumbi mwezi ujao huku bingwa mtetezi akiwa ni Yanga akiwa
amechukua ubingwa mara 36, akifuatiwa na
Simba ikiwa amechukua mara 18.
Tazama Kifaru akielezea usajili batiri wa Mbonde katika Klabu ya simba hapo chini
Tazama Kifaru akielezea usajili batiri wa Mbonde katika Klabu ya simba hapo chini


No comments:
Post a Comment